Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

MKURUGENZI WA FEMAPO MATHIAS LYAMUNDA AMECHANGIA MILIONI 1 SHULE YA MSINGI BAHI



Na. Kadala Komba Bahi

Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO), amechangia Shilingi Milioni moja (1,000,000/: taslimu kwajili ya maendeleo ya shule ya  Msingi Bahi Mission na Shule ya Msingi ya Chiona.

Hayo yamejiri wakati wa Mahafali ya 92 katika Shule hizo mbili ambazo zimefanya vizuri na kushika nafasi ya kwanza na ya Pili Kiwilaya na Kimkoa.

Akizungumza katika Mahafali hiyo Mathias Lyamunda aliyepewa heshima ya kuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya 92 ya Shule hizo ambazo  zimekuwa na ufaulu mzuri  Kiwilaya na kuweka wilaya ya Bahi nafasi ya 2 kitaifa baada ya Kinondoni ya Mkoa wa Dar es salaam.


Sambamba na hilo Mathias Lyamunda  amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha nyingi  kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Bahi  aliwapongeza wanafunzi,  walimu na wazazi kwa ushirikiano wao mzuri ambao umepelekea kupatikana kwa ufaulu mzuri katika shule hizo mbili,na  kusisitiza umuhimu wa jamii kuwalinda watoto wa Kiume na wa Kike kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili kwa watoto, ambavyo alisema tafiti zinaonesha asilimia 80% ya matukio ya ukatili kwa watoto yanafanya na watu waliokaribu na familia ya mtoto. Amesisitiza yeye kama mdau mkubwa wa ulinzi wa mtoto anapinga vitendo hivyo na ameiasa jamii kuchukua hatua kuwalinda watoto kwani watotoni Taifa la Sasa na la kesho.

MWISHO

Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO), Akizungumza katika Mahafali

 

Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO), Akiwasili Viwanja vya Shule ya Msingi Bahi alipokelewa na Mwalimu Mkuu wa Bahi Misheni , Paschal Andrea Mchewa.



Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO),akifungwa kiskafu na Vijana wa Skauti

Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO), Akikabidhi vyeti kwa Walimu wa shule ya msingi Bahi misheni na Chiona


Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO),Akimlisha keki mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bahi Misheni



Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO),Akiwapa vyeti wahitimu wa Darasa la saba




*FURSA KWA WANAWAKE KUKOPA DOWOSA RIBA ASILIMIA 1 KWA MWEZI*


Na. Kadala Komba Dodoma

Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Amewataka wanawake kujiunga na DODOMA WOMEN SACCOS (DOWOSA) kwa maendeleo ya uchumi wetu Dowosa ni Saccos ya kujiunga ninauhakika kwa Dowosa ni chombo cha kuchochea kukuwa kwa uchumi katika jamii na Taifa wanachama na viongozi zingatieni mambo muhimu hili chama kiwe endelevu Alisema .
"Hivyo toweni Elimu ya  kutosha kwa wanawake waweze kujiwekea hakiba ya kila mwezi na ununuzi wa hisa kwani uwekezaji mdogo wa hisa unaasili mtaji wa Saccos.

Hayo yamejiri wakati Mkutano Mkuu wa pili wa Dodoma Women Saccos Limited mwishoni mwa wiki katika  Jengo la Hazina Ukumbi wa Kambarage -Wizara ya Fedha Dodoma.

Mhe. Mbonipaye Mpango alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya hawamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu kwa kuweka mazingira rafiki ya uwazishwaji na uendeshaji wa Saccos ambayo  imewezesha Dowosa kuanzishwa kama Saccos nyingine Dowosa itaenda kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika ngazi ya familia ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla kutokana na uraisi wa kupata huduma za fedha kwa gharama nafuu asilimia 1 nisawa na bure unakopa milioni Ishirini (20 )unalipa laki mbili  (2 ) kwa mwezi ni fedha ndogo sana imani yangu wanawake wengi watahamasika kujiunga na Dowosa.


Naye Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule  Amempongeza Amempongeza Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa kipaombele kwenye mambo ya wanawake sio wanawake wa Dodoma tu ila nchi nzima umekuwa na upendo na wanawake nimeona Sehemu nyingi unazokaribishwa unakuwa nao bega kwa bega tunakushukuru sana ili linaonesha kabisa unafurahia maendeleo ya wanawake.

Kwaupende wake Kitorina Kipa Mwenyekiti Dodoma Women Saccos alisema  malengo ya kuanzisha Saccos hii ni kuwakwamua wanawake kiuchumi kutokana na wanawake wengi wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa kutokana na kukopa mikopo kwenye baadhi ya taasisi za fedha zenye masharti magumu na Riba kubwa.

Alisema wanawake wengi hasa wajasiriamali wadogo wamekuwa wakinyanyasika sana wengine kuuziwa vitu vyao vya ndani na wengine kuvunjika kwa ndoa zao na wengine kupoteza kupoteza maisha kutokana na kushindwa kulipa mikopo hiyo maalufu kausha Damu au mikopo umiza, hivyo Saccos hii imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wanawake wajasilimali wa Dodoma kupata mikopo kwa masharti nafuu na kwa riba ndogo ya Asilimia moja (1) tu kwa mwezi alisema .


MWISHO 



Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa pili wa Dodoma Women Saccos Limited
 


Kulia Kitorina Kipa Mwenyekiti Dodoma Women Saccos katikati ni Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule Nyuma ni Bodi ya Bodi ya Dodoma Women Saccos Limited

Kitorina Kipa Mwenyekiti Dodoma Women
Akisoma risala kwa Mgeni Rasmi
 

Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule Akimkabidhi Zawadi Mgeni Rasmi Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania    



Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule Akitazama Zaidi aliyokabidhiwa na Dodoma Women Saccos Limited



Wanachama wa Dodoma Women Saccos Limited kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka



Mwenyekiti wa muda wa mkutano  AZiza Mumba

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dododoma Mhe.Fatma Toufiq Akipokea cheti cha Mkopaji Bora

Bodi ya Dodoma Women Saccos Limited

*ENDELEENI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI” MHE. NDERIANANGA*

 

Na Mwandishi wetu - Dodoma

 


 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameihimiza jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI nchini kwa kuendelea kuzingatia elimu inayotolewa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) ili kuunga mkono jitihada za Serikali dhidi ya mapambano hayo na kuyafikia malengo yaliyopo.

Mhe. Nderiananga ametoa wito huo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Tano wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI wa mwaka 2021/22 hadi 2025/26 iliyowasilishwa leo tarehe 21 Oktoba 2024 katika ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa tume hiyo Dkt. Jerome Kamwele katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI.

Alisema, jamii haina budi kuendelea kujilinda na kuwalinda wengine kwa kuzingatia ushauri na elimu inayotolewa ili kuhakikisha hali ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI nchini ipungue na kuyafikia malengo ya kuzifikia sifuri tatu ifikapo 2030.

“Suala la UKIMWI siyo la TACAIDS na Ofisi ya Waziri Mkuu peke yake, Wizara ya Afya inapambania kuboresha huduma ya mama na Mtoto, Ofisi ya Rais TAMISEMI ndio imejenga miundombinu  na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewekeza Ujenzi hadi ngazi ya Kata kuna vituo Vya afya yote hii ni kusogeza huduma karibu na wananchi na uwekezaji huu tutaona matunda yake katika mapambano dhidi  ya VVU,”Alieleza Mhe. Nderiananga.

Pia aliishukuru TACAIDS kwa kufanya kazi nzuri ya kuifikia jamii kwa njia ya elimu huku akiwahimiza kuendelea kuongeza nguvu kwa vijana kwani ndilo kundi linaloongoza kwa maambukizi bila kusahau ni kundi muhimu katika uzalishaji na kujiletea maendeleo.

Awali akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa Mkakati wa Tano wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI wa mwaka 2021/22 hadi 2025/26 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa tume hiyo Dkt. Jerome Kamwele alieleza kwamba, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi Oktoba 2024, tume hiyo imefanikiwa kuratibu kwa ufanisi utekelezaji wa mkakati katika sekta zote ndani ya Serikali na sekta binafsi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Taasisi za dini na wadau mbalimbali.

“Tume pia tumefanikiwa kupunguza maambukizi mapya ya VVU kutoka maambukizi 61,281 mwaka 2020 hadi maambukizi 60,000 mwaka 2023, kupungua kwa vifo vitokanavyo na UKIMWI kutoka vifo 32,639 mwaka 2020 hadi vifo 25,000 mwaka 2023 na kupungua kwa kiwango cha ubaguzi na unyanyapaa unaogokana na VVU kutokana na elimu ambayo imeendelea kutolewa kwa jamii na wadau,” alieleza Dkt. Kamwele.

Alifafanua kwamba mafanikio mengine ni pamoja na kufikia lengo la utekelezaji wa shabaha za Kimataifa 95-95-95 zinazohusu kupima na kutibu ifikapo 2026 ambapo asilimia 98 ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI  (WAVIU) wameanza tiba huku utafiti ukionyesha mwelekeo mzuri wa kufikia shabaha ya asilimia 95 ya tatu inayohusu kufubaza Virusi vya UKIMWI na kusisitiza ushirikiano wa pamoja kufikia asilimia 95 ya kwanza inayohusu watu wote wanaoishi na VVU kupima na kujua hali zao.

“Serikali inaendelea kuweka mkazo katika utekelezaji wa afua zinazolenga kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya VVU hasa makundi maalum, kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha watu kupima kujua hali zao, kuongeza nguvu kuyafikia makundi maaalum hasa vijana, wanawake, wanaume, Watoto, watu wenye ulemavu na wanaoishi katika mazingira hatarishi,” alifafanua.

Aidha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Bernadeta Mushashu aliipongeza TACAIDS kwa jitihada zake ikishirikiana na wadau kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao za kiuchumi wakiwa katika hali njema ya kiafya.

MWISHO

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Tano wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI wa mwaka 2021/22 hadi 2025/26 iliyowasilishwa leo tarehe 21 Oktoba 2024 katika ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa tume hiyo Dkt. Jerome Kamwele katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI.





UCHAGUZI MWAKA 2024\2025 UMEWAKUTANISHA WADAU WA SIASA NA VIONGOZI WA DINI

Na. Kadala Komba Bahi 

Mkurugenzi wa wilaya na msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Bahi Mhe. Zaina Mlawa ametoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa uchaguzi,kuanzia hatua ya kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura. 

Hayo yamejiri wakati wa mkutano wa kikao kazi cha  wadau wa vyama vya siasa na viongozi wa dini kikao  kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wilayani Bahi Septemba 26\09\2024 alisema kwa mujibu wa kanuni ya 27 GN. Na. 571 Kampeni za uchanguzi zitaanza tarehe 20 hadi tarehe 26 Novemba 2024 .

 Aidha Mkurugenzi  Mlawa amesema kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ni hatua muhimu inayompa kila mwananchi mwenye sifa haki ya kisheria kushiriki uchaguzi kama mpiga  kura au mgombea hivyo wananchi nawahimiza kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kutumia haki yako ya kupiga kura au kugombea nafasi za uongozi.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi amesema Ushiriki wa wananchi wengi katika kugombea nafasi za uongozi ni muhimu katika kukuza demokrasia na kuhakikisha upatikanaji wa viongozi bora kwa maendeleo ya taifa letu .
 

 
Upande wa kulia ni
Mkurugenzi wa wilaya na msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Bahi Mhe. Zaina Mlawa kushoto kwake ni Michael Ziwa Afisa Uchaguzi Bahi.
 
 
 
Mkurugenzi wa wilaya na msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Bahi Mhe. Zaina Mlawa akipitia tangazo la uchanguzi.

 
 
 
Picha ni Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Bahi Paulina Deus Bupamba
 
 
Picha ni Shekh Ramadhani Utengule akizungumza namna alivyopokea tanagzo la uchanguzi kama kiongozi wa kiislamu


Kasisi wa kanisa la Anglikana parishi ya Bahi Nason Mjimbu,Akielezea namna ambavyo wamepokea Tangazo la uchanguzi 

Katibu Uvccm wilaya ya Bahi Hussein Muya akizungumza namna ambavyo chama mapinduzi kilivyo jipanga katika utekelezaji wa zoezi la kujiandikisha kupiga kura .



 
 
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la FPCT Bahi
Peter  Sponga  akijitambulisha katika mkutano
 



Katibu UWT wilaya ya Bahi Hilda Mdaki akijitambulisha wakati wa  mkutano wa kikao kazi cha  wadau wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.