Na. Kadala Komba Bahi
Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO), amechangia Shilingi Milioni moja (1,000,000/: taslimu kwajili ya maendeleo ya shule ya Msingi Bahi Mission na Shule ya Msingi ya Chiona.
Hayo yamejiri wakati wa Mahafali ya 92 katika Shule hizo mbili ambazo zimefanya vizuri na kushika nafasi ya kwanza na ya Pili Kiwilaya na Kimkoa.
Akizungumza katika Mahafali hiyo Mathias Lyamunda aliyepewa heshima ya kuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya 92 ya Shule hizo ambazo zimekuwa na ufaulu mzuri Kiwilaya na kuweka wilaya ya Bahi nafasi ya 2 kitaifa baada ya Kinondoni ya Mkoa wa Dar es salaam.
Sambamba na hilo Mathias Lyamunda amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Bahi aliwapongeza wanafunzi, walimu na wazazi kwa ushirikiano wao mzuri ambao umepelekea kupatikana kwa ufaulu mzuri katika shule hizo mbili,na kusisitiza umuhimu wa jamii kuwalinda watoto wa Kiume na wa Kike kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili kwa watoto, ambavyo alisema tafiti zinaonesha asilimia 80% ya matukio ya ukatili kwa watoto yanafanya na watu waliokaribu na familia ya mtoto. Amesisitiza yeye kama mdau mkubwa wa ulinzi wa mtoto anapinga vitendo hivyo na ameiasa jamii kuchukua hatua kuwalinda watoto kwani watotoni Taifa la Sasa na la kesho.
MWISHO
Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO), Akizungumza katika Mahafali |
Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO), Akikabidhi vyeti kwa Walimu wa shule ya msingi Bahi misheni na Chiona