Subscribe Us

CHANGAMOTO YA WASICHANA KUACHA SHULE BADO IPO

 
Na Sifa Lubasi, Chemba 



UTAFITI wa tathimini uliofanywa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/met) umeonesha changamoto ya kuacha shule bado ipo kwa wasichana kwa asilimia  saba kwa shule za msingi na asilimia tano kwa shule za sekondari katika Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Hayo yamebainika  wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi  wa Kuondoa vizuizi vya elimu kwa wasichana na wavulana ili kupunguza kuacha shule(utoro), kuongeza idadi ya wasichana na wavulana wanaobakia shuleni na kuboresha kiwango cha kukamilisha masomo na ufaulu.
Mradi huo unatekelezwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Woman Wake Up (Wowap) ambapo msimamizi wa mradi ni Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/met)na mfadhili wa mradi huo kwa awamu ya kwanza na ya pili ni Malala Fund.
Msimamizi wa miradi wa Ten/met, Kenneth Nchimbi alisema kuwa  utafiti wa tathmini ya mwisho ulionyesha kuwa mipango ya mradi ilifanikiwa kuchangia kufikia matokeo yanayotarajiwa; kama kupunguza kiwango cha wanafunzi wanaoacha shule, hasa kwa wasichana, lakini changamoto ya kuacha shule bado ipo kwa wasichana kwa asilimia saba kwa shule za msingi na asilimia tano kwa shule za sekondari
Alitaja maeneo machache yanayohitaji juhudi zaidi ni pamoja na mafunzo zaidi ya stadi za maisha, kampeni za uelewa kwa wazazi, mikakati ya kudumisha vilabu vya shule, na kuhusisha wavulana katika vilabu kwani wanahisi kubaguliwa na mara nyingine husababisha matatizo kwa wasichana.
Alisema kuwa ushahidi wa tathmini ya mwisho ulionyesha kuwa mipango ya mradi ilifanikiwa kuchangia kufikia matokeo yanayotarajiwa; kama kupunguza kiwango cha wanafunzi wanaoacha shule, hasa kwa wasichana.  
Alisema kuwa awamu ya kwanza ilikuwa na shule sita; awamu ya pili inaongeza shule mbili zaidi hivyo kufikia shule nane.
"Awamu ya kwanza ilikuwa na shule sita ambazo ni Kelema Maziwani (Msingi), Kwa Mtoro(Sekondari), Soya(Msingi), Mrijo(Sekondari),Mrijo(Msingi), na  Soya(Sekondari katika awamu ya pili  shule zilizoongezeka ni Kelema Balai(Msingi), na Chemba (Sekondari)," alisema
Alisema kuwa awamu ya pili ya mradi utafiti wa tathmini ya mwisho ulionyesha kuwa mafunzo ya stadi za maisha yaliyotolewa katika vilabu vya shule, pamoja na ziara za kujifunza, zillikuwa muhimu katika kuwawezesha wasichana kuvuka vikwazo katika elimu yao.
Mratibu wa miradi kutoka Wowap, Nasra Suleiman alisema kuwa utafiti uliofanyika baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya radi umeonesha ufanisi ndio sababu iliyopelekea mradi huo kutekelezwa kwenye awamu ya pili.
mwisho

0 Comments:

Post a Comment