Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

“SERIKALI KUJENGA VITUO MAALUM VYA UREKEBU” WAZIRI MHAGAMA


Na; Mwandishi Wetu – Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, amesema  Serikali imejenga vituo maalum vya urekebu na ufundi stadi ili kuwasadia vijana  na wale wote wanaoathirika baada ya kutumia dawa za kulevya.

Ameyasema hayo mapema leo Mei 30 2023, Bungeni  Dodoma  wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 ambapo amessema kwa mujibu wa utafiti unaonyesha  uwepo wa kiwango kikubwa cha uzalishwaji na ulimaji wa bangi.

Waziri Mhagama alisema, kwa mwaka ujao wa  fedha  2023/2024 Serikali imetenga bajeti ya shilingi Bilioni nane nukta saba (Bilioni 8.7)  zitakazotumika kujenga vituo vya urekebu na ufundi stadi, vitakavyosaidia kubadilisha tabia za vijana wanaotumia dawa  za kulevya,

 “Vituo hivyo vitakuwa na kazi kubwa ya kuwaondoa kwenye matumizi ya dawa na kuwapa shunguli nyingine watakazotakiwa kuzifanya zitakazotokana na shughuli za ujuzi, ambazo watafundishwa kwenye vitu hivyo.” Alifafanua.

Aliendelea kusema kuwa, kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali itafanya utafiti, ili maeneo yanayolima bangi kibiashara kama vile Kisimiri Juu mkoani Arusha, kusaidiwa kulima mazao mbadala na juhudi za Serikali za kukomesha kilimo hicho zinaweza kuwasaidia kutoka kwenye biashara hiyo haramu kwa makusudi ya kuongeza kipato, na kuwafanya vijana na watumiaji kuwa salama.

“Kwa Jiji la Dodoma pekee tunategemea kutumia kiasi cha shilingi Bilioni mbili, kujenga kituo hicho katika Eneo la Itega.” Alisema.

Awali akiongea katika mkutano huo na waandishi wa habari aliitaja baadhi ya  mikoa inayoongoza kwa kulima bangi nchini kuwa ni pamoja na Arusha, Manyara, Mara na Njombe,na kuitaja baadhi ya Mikoa itakayojengwa vituo hivyo kuwa ni pamoja na Shinyanga, Kilimanjaro, Mwanza  na Arusha.

###MWISHO####


Waziri  wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa Taarifa  kuhusu  hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 kwa waandishi wa habari tarehe 30 Mei, 2023 Jijini Dodoma
 

TUKUMBUKE KULIOMBEA TAIFA - SIMBACHAWENE

 Na. Mwandishi Wetu.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya  Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewataka viongozi wa dini zote nchini kuendelea kuliombea Taifa amani, utulivu  pamoja na kukemea vitendo viovu vya mmomonyoko wa maadili vinavyoendelea duniani kote.
 
Waziri Simbachawene ameyasema hayo wakati alipomuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa katika Ibada ya Harambee ya uchangishaji fedha katika Usharika wa Kongwa, Dayosisi ya Dodoma ambapo ameahidi kuchangia milioni kumi kwa ajili ya kumalizia jengo la Kanisa hilo huku akimbatana na viongozi mbalimbali wa Mkoa  wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Mhe. Job Ndugai.
 
"Mhe. Rais amekuwa akitoa wito kila siku ya kwamba mara zote tukumbuke kuiombea nchi yetu iwe na amani, mshikamano, ustawi, mafanikio na maendeleo lakini pia tuliombee Taifa letu ili kuepukana na mmomonyoko wa maadili ambao unaathiri Utamaduni wa Taifa letu niwaombe msiache kuliombea kila mnapofanya ibaada zenu" Amesema Simbachawene
 
Akitoa salamu za Serikali Simbachawe ametoa rai kwa waumini hao kuiombe nchi amani, upendo, utulivu na mshikamano kwakuwa nakusisitiza kuwa ustawi wake ndio chachu ya maendeleo
 
Mhe. Simbachawene pia ametumia fursa hiyo kukukemea vikali kuhusu mmonyoko wa maadili, mahusiano ya ndoa za jinsia moja na kuwaasa waumini kusimama katika maagano ya Mungu na kuwaomba maaskofu kuendelea kukemea na kuomba kwakuwa hakuna sababu za kuogopa.
 
Simbachawene amesema Serikali inatambua mchango wa Kanisa katika kukuza sekta ya Elimu, Afya na Maendeleo ya jamii kwa kuwa kichocheo kikubwa katika kutukuza neno la mungu kupitia huduma wanazotoa.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewapongeza waumini wa usharika huo kwa kuendelea na ujenzi wa kanisa hilo ambao ujenzi wake unagharimu zaidi ya Shilingi milioni 360 hadi kukamilika kwake ambapo hadi sasa zaidi ya Shilingi millioni 203  zimekwishatumika.
 
"Hongereni sana kwa hatua mliyofikia ya ujenzi mmefika sehemu nzuri, mmeangalia Dodoma kama Makao Makuu ya Nchi na nyie mmejenga Kanisa la kimakao Makuu kweli kweli niwapongeze sana na Mungu awabariki" amesema Mhe. Senyamule
 
Naye Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Dodoma Christian Ndossa amesema Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuonyesha ushirikiano kwa madhehebu mbalimbali huku akiwataka watanzania kuacha uvivu wa kusoma na kusikiliza neno la Mungu na kukimbilia  miujiza  isiyo na kweli ndani yake.
 
Askofu huyo amesema shina la uharibifu limesimama hivyo wanadamu wamepotea kwa kukosa maarifa, na kutoa rai kwa waumini kurarua mioyo yao na si mavazi.
 
"Tusimame katika nafasi zetu kwa kusimamia maandiko matakatifu na kuendelea kumuomba Roho Mtakatifu kusaidia katika kufanikisha mambo ambayo kwa macho ya kibinadamu yanaonekana hayawezekani" Amesisitiza Askofu Ndossa
 
Takriban kiasi cha shilingi Milioni 77.8 kimepatikana kupitia harambee hiyo na mifuko 270 ya saruji kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa jengo hilo la kanisa la KKKT Dayosisi ya Kongwa.







CHANGAMOTO YA WASICHANA KUACHA SHULE BADO IPO

 
Na Sifa Lubasi, Chemba 



UTAFITI wa tathimini uliofanywa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/met) umeonesha changamoto ya kuacha shule bado ipo kwa wasichana kwa asilimia  saba kwa shule za msingi na asilimia tano kwa shule za sekondari katika Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Hayo yamebainika  wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi  wa Kuondoa vizuizi vya elimu kwa wasichana na wavulana ili kupunguza kuacha shule(utoro), kuongeza idadi ya wasichana na wavulana wanaobakia shuleni na kuboresha kiwango cha kukamilisha masomo na ufaulu.
Mradi huo unatekelezwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Woman Wake Up (Wowap) ambapo msimamizi wa mradi ni Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/met)na mfadhili wa mradi huo kwa awamu ya kwanza na ya pili ni Malala Fund.
Msimamizi wa miradi wa Ten/met, Kenneth Nchimbi alisema kuwa  utafiti wa tathmini ya mwisho ulionyesha kuwa mipango ya mradi ilifanikiwa kuchangia kufikia matokeo yanayotarajiwa; kama kupunguza kiwango cha wanafunzi wanaoacha shule, hasa kwa wasichana, lakini changamoto ya kuacha shule bado ipo kwa wasichana kwa asilimia saba kwa shule za msingi na asilimia tano kwa shule za sekondari
Alitaja maeneo machache yanayohitaji juhudi zaidi ni pamoja na mafunzo zaidi ya stadi za maisha, kampeni za uelewa kwa wazazi, mikakati ya kudumisha vilabu vya shule, na kuhusisha wavulana katika vilabu kwani wanahisi kubaguliwa na mara nyingine husababisha matatizo kwa wasichana.
Alisema kuwa ushahidi wa tathmini ya mwisho ulionyesha kuwa mipango ya mradi ilifanikiwa kuchangia kufikia matokeo yanayotarajiwa; kama kupunguza kiwango cha wanafunzi wanaoacha shule, hasa kwa wasichana.  
Alisema kuwa awamu ya kwanza ilikuwa na shule sita; awamu ya pili inaongeza shule mbili zaidi hivyo kufikia shule nane.
"Awamu ya kwanza ilikuwa na shule sita ambazo ni Kelema Maziwani (Msingi), Kwa Mtoro(Sekondari), Soya(Msingi), Mrijo(Sekondari),Mrijo(Msingi), na  Soya(Sekondari katika awamu ya pili  shule zilizoongezeka ni Kelema Balai(Msingi), na Chemba (Sekondari)," alisema
Alisema kuwa awamu ya pili ya mradi utafiti wa tathmini ya mwisho ulionyesha kuwa mafunzo ya stadi za maisha yaliyotolewa katika vilabu vya shule, pamoja na ziara za kujifunza, zillikuwa muhimu katika kuwawezesha wasichana kuvuka vikwazo katika elimu yao.
Mratibu wa miradi kutoka Wowap, Nasra Suleiman alisema kuwa utafiti uliofanyika baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya radi umeonesha ufanisi ndio sababu iliyopelekea mradi huo kutekelezwa kwenye awamu ya pili.
mwisho

Leseni 3,214 madereva mabasi, malori zafutwa

 

JESHI la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani limezifuta leseni 3,214 za madaraja C na E za madereva waliokuwa wakiendesha malori na mabasi ya abiria.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Ramadhani Ng’anzi amesema Dar es Salaam jana kuwa leseni zilizofutwa ni kati ya leseni 20,940 zilizohakikiwa hadi Aprili 30, mwaka huu.

Kamanda Ng’anzi alilieleza HabariLEO ofisini kwake kuwa madereva waliokuwa wakimiliki leseni hizo hawana sifa ikiwamo ya kusomea madaraja hayo.

Alisema leseni zilizofutwa zilionekana kutokidhi vigezo kwa sababu wahusika wamezipata visivyo halali na wameshushwa madaraja hadi ya awali ambayo ni D na B.

Kamanda Ng’anzi alisema leseni 17,726 zilibainika kuwa zimekidhi vigezo na hadi sasa wamehakiki asilimia mbili ya leseni za madereva wa madaraja C na E.

Alisema uhakiki awamu ya kwanza ulianza Machi Mosi kwa hiari kwa madereva kutakiwa kufika ofisi za wakuu wa usalama barabarani kuhakiki leseni zao na kazi hiyo ilipangwa kukamilika Aprili 30, mwaka huu.

Kamanda Ng’anzi alisema wameongeza muda hadi Julai 31, mwaka huu ili kutoa nafasi kwa madereva kusomea madaraja E na C kwa sababu kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu za jeshi, ni lazima dereva apite katika shule za udereva.

“Niliwaambia wakuu wa usalama barabarani madereva wasibuguziwe tuwaache wenyewe waje kwa hiyari ila tukianza kuwapekuwa na kuwakamata tutawauliza na kuwahoji katika kipindi hiki tulichokuwa tumetoa muda wa kuhakiki wa hiyari walikuwa wapi kuhakiki,” alisema Kamanda Ng’anzi.

Mwishoni mwa Februari mwaka huu, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali Camilius Wambura alilifuta Dawati la Leseni la Jeshi la Polisi baada ya kubaini kuna ukiukwaji wa maadili.

Baada ya uamuzi huo, liliundwa dawati jipya la utoaji wa leseni na kikosi kilitakiwa kuhakiki ni leseni zipi zilipatikana kiuhalali na zipi hazikufuata utaratibu na kujua dereva gani ni mahiri katika eneo lake la ka


AFUTA HARUSI BAADA YA MCHUMBA KUMPELEKEA X WAKE KADI YA MUALIKO NA KUPAKULIANA ASALI

 Mwanamke mmoja raia wa Nigeria amejawa na machozi baada ya mchumba wake kufuta harusi yao.


Mrembo huyo alianika suala hilo kwenye kundi la Facebook na kuomba ushauri wa wanamtandao.

Alisema alimtembelea tu mpenzi wake wa zamani ili kumpa kadi ya mwaliko kwenye harusi yake, lakini aliishia kurusha roho na jamaa huyo.

Kwa bahati mbaya, mume wake mtarajiwa aligundua kuhusu uzinzi wake baada ya kudukua simu yake.

Baadaye mwanaume huyo aliagiza kwamba matayarisho yote ya harusi yasitishwe mara moja. 

Mrembo huyo alilalama kuwa: "Mbele yangu, aliwaita wazazi wote wawili na kuwataka wasitishe maandalizi yote ya harusi. Walipouliza kwanini, aliwaambia nitaeleza vizuri zaidi. Aliniacha nyumbani kwake na kwenda hotelini na hakurudi" 

Maoni ya wanamtandao 

Kingsley Uchenna alisema: "Upuuzi. Kwa nini ulikubali mtoto wa mtu wakati bado unampenda ex wako? Maisha haya EEE. Mwanaume amefanya vizuri. Anaamini unaweza kufanya zaidi atakapokuoa!"

@Adeoye Augustine Okusanya alitoa maoni: "Kwa nini ulishuka chini namna hii? Ni kama bado una hisia ya kimapenzi na mpenzi wako wa zamani."




AMUUA MKE MWENZA KWA KUMCHOMA SINDANO YA SUMU

 Maafisa wa Polisi nchini Uganda wanamsaka mwanamke anayedaiwa kutoroka nyumbani baada ya kumchoma mke mwenza kwa sindano iliyokuwa na sumu.


Jackie Namubiru anadaiwa kumuua mke mwenza Nakimera Lydia mwenye umri wa miaka 23, baada ya kumdunga sindano yenye sumu na kutoroka. 

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na jarida la Nilepost, Lydia alikimbizwa katika Kliniki ya Bulamu na kuhamishwa hadi Hospitali ya Byansi iliyoko Masaka baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.

"Mwathiriwa aliaga dunia kwa kutiliwa sumu mwilini mnamo Aprili 24, 2023 saa kumi na mbili  na nusu jioni,” msemaji wa polisi Fred Enanga alisema siku ya Jumanne.

Enanga aliongeza kusema kwamba tukio hilo huenda lilitendeka kutokana na wivu baina ya wake wenza hao na kwa sasa mshukiwa anasakwa vikali na maafisa wa polisi.




SEKTA YA UVUVI NA KILIMO NI UTAJIRI

NA.MWANDISHI WETU

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema sekta ya kilimo na uvuvi zinatija katika kujiletea maendeleo ya taifa letu kwa kuzingatia fursa zilizopo.

 

Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya Kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP inayoratibiwa na ofisi yake Mkoani  Morogoro.

 

Dkt. Yonazi alitembelea baadhi ya Wilaya zinazotekeleza mradi huo ikiwemo Morogoro Mjini na Kilosa ambapo alikagua utekelezaji huo katikaTaasisi ya Utafiti wa Mbegu (TIRA), Taaasisi ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu (TOSCI) pamoja na Kituo cha Viumbe Maji (DAQ) kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

 

Alifafanua kuwa Tanzania inautajiri mwingi kupitia fursa zinazotokana na sekta hizo huku akieleza kuwa nchi ya Tanzania itakuwa kituo cha maarifa ya kujifunza kilimo na uvuvi kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana na jitihada za Serikali katika kuwekeza katika sekta hizo.

Aliongezea kuwa kupitia mradi wa kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi utasaidia kuendelea kuboresha miundombinu muhimu kwa lengo la kuhakikisha ufugaji unakuwa sehemu ya pato la taifa na kuchangia kasi ya maendeleo pamoja na kuliingizia taifa fedha za kigeni.

 

“Tanzania imeendelea kuwekeza katika sekta ya uvuvi na kilimo, na hii itaipa nafasi nchi yetu kuwa kituo cha maarifa ya kujifunza masuala ya kilimo na nchi zinazotuzunguka, ni muda sahihi kuendelea kuweka nguvu zaidi kwa kuzingatia mazingira yetu ya uwekezaji,”alisema

 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuleta miradi hiyo katika mkoa wake huku akiitaja Morogoro kwa mafanikio makubwa eneo la kilimo na uvuvi kwa kuzingatia ardhi yenye rutuba kwa mkoa wa Morogoro.

 

“Mkoa wetu una mvua nyingi na umeendelea kuwa mzalishaji mzuri wa mazao ikiwemo mpunga. Tumeendelea kuwa wa kwanza kwa uzalishaji wa mpunga nchini,  namba sita kwa uzalishaji wa ndizi, namba nne kwenye G5 katika uzalishaji wa chakula nchini, malengo yetu ni kufanya vizuri zaizi ili kusogea kutoka nafasi ya nne kitaifa kuwa nafasi nzuri zaidi,”Mhe. Mwassa

 

Aliongezea kuwa, mkoa wake umeendelea kutoa kipaumbele katika masuala ya kilimo kwa kuendelea kutenga bajeti.

 

Awali akieleza lengo la mradi wa AFDP Mratibu wa program hizo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Salimu Mwijaka alisema, hadi sasa mradi umefikia mikoa 11 ikiwemo; Morogoro, Geita, Lindi,Tanga, Pwani, Dodoma, Singida, Manyara,Tabora, Geita, Shinyanga na Mwanza na kueleza umejipanga kufanya vizuri kwa matokeo yenye tija.

 

“Mradi huu umejikita katika maboresho maeneo mengi ikiwemo ya kuboresha networking ya distribution ya mbegu, na kuhakiksiha tunaboresha maeneo ya umwagiliaji, upatikanaji wa vifaa kama matrekta katika mashamba, udhibiti wa mbegu katika maabara aidha upande wa samaki tumeendelea kujenga na kuongeza uwezo wa vitotoreshi vya vifaranga vya samaki, kuboresha mabwawa ya kufugia samaki,“alisema Mwijaka

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kituo cha Ukuzaji viumbe Maji cha Kingolwira Bi.Gillness silayo alieleza faida za program ambayo utaleta unafuu kwa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo uchakavu wa mabwawa na ukosefu wa maji.

“Mradi IFAD utatusaidia kuboresha mabwawa yetu 20 hivyo kuongeza makusanyo ya maduhuri, pamoja na hilo mradi utatuchimbia visima vitavyotatuta changamoto ya maji katika ufugaji wa samaki,”alisema Gillness

=MWISHO=




Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akiangalia mbegu za alizeti wakati wa ziara yake katika kalakana ya kuchakata mbegu za mazao ya Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) alipotembelea katika mkoa wa Morogoro.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akikagua mbegu za mpunga zilizohifadhiwa katika vifungashio katika mashine za kuchakata mbegu za kilimo za Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kilichopo katika Mkoa wa Morogoro.








Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi  akizungumza wakati wa kikao chake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa alipomtembelea ofisini kwake wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua utekelezaji wa program ya Kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP inayoratibiwa na Ofisi yake mkoani Morogoro.





Mkurugenzi wa Uzalishaji Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Dkt. Justine Ringo akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi mitambo ya kuchakata mbegu za kilimo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa program kuendeleza kilimo na uvuvi inayoratibiwa na ofisi yake.





Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akioneshwa vifungashio vya mbegu na Mtendaji Mkuu Taasisi ya Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Dkt. Sophia kashenge wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Program ya kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi inayoratibiwa na ofisi yake.Ziara hiyo ilifanyika mkoani Morogoro.




Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi pamoja na timu aliyoongozana nayo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya katibu mkuu huyo kukagua utekelezaji wa program ya Kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP katika mkoa wa Morogoro.



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi (mwenye suti ya blue) pamoja na timu aliyoongozana nayo wakikagua moja ya bwawa la kuhifugia samaki lililopo katika Kituo cha Viumbe Maji (DAQ) kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa program ya AFDP.




 

 



 



WAJAWAZITO KUPIMWA VIPIMO VYA AWALI BILA MALIPO

Na. Catherine Sungura-Dodoma.

 
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amewataka akina mama wajawazito wanaofika kwenye Kliniki za Uzazi, Mama na Mto kupimwa wingi wa damu, mkojo kuangalia wingi wa protini, shinikizo la damu pamoja na kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto bila kutozwa gharama zozote.
 
Haya ameyasema leo wakati wa kukabidhi  vifaa tiba vya kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto kwa vituo  ishirini vya halmashauri za Mkoa wa Dodoma vyenye thamani ya Shilingi milioni 45 .
 
Waziri Ummy amesema kuwa vipimo hivyo ni muhimu kwa wajawazito ili kuweza kuepusha kifafa cha mimba na vifo  kwa wajawazito.
 
“Ili kuweza kumuokoa mama mjamzito anapofika kliniki ni vyema kupimwa vipimo hivyo muhimu, vipimo hivi vyote ni bure na ni lazima viwepo  kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vyote nchini.
 
Aidha, waziri Ummy amesema Serikali itahakikisha  upatikanaji wa 100% wa dawa za kuzuia kutoka damu wakati wa kujifungua, dawa za kuongeza damu na dawa za kuzuia kifafa cha mimba katika vituo vya afya vya umma nchini.
 
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatimiza wajibu wake kwa kujenga majengo,kuboresha miundombinu, kuongeza ajira  pamoja na kununua vifaa tiba , hivi sasa tunapata fedha za dawa kila mwezi shilingi bilioni 20, tutahakikisha hizi dawa tatu zitapatika kwa asilimia 100”. Amesema Mhe. Ummy
 
Hata hivyo Waziri Ummy amezitaka Timu za afya za uendeshaji  za Halmashauri nchini kufanya usimamizi shirikishi  kwenye vituo vya kutolea huduma za afya  ili kuwajengea uwezo watoa huduma  za afya, “Huu ndio muelekeo wa wizara, twende kwenye masuala  ya kuwawezesha wataalamu wetu kwenye vituo vya afya na kuona kipi kinafanyika tunaweza kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga kama tutaongeza kutoa huduma bora za afya”. Alisisitiza.
 
Akitaja taarifa za Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya na Utafiti wa Kiashiria cha Malaria (DHS/MIS) ya mwaka 2022 zinaonesha kuwa nchi imepiga hatua katika viashiria vingi vya afya vya mama na mtoto mathalani vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimeshuka  kutoka 67 kati ya vizazi hai 1000 mwaka 2015/2016 hadi 43 kwa kila vizazi  hai 100.
 
“Mahudhurio kliniki ya wajawazito mara nne na zaidi kutoka 53% hadi 65%, aidha, wajawazito  wanaojifungulia  katika vituo vya huduma wameongezeka kutoka 63% hadi 81% na wanaojifungua chini ya uangalizi wa mtoa huduma mwenye ujuzi kutoka 66% hadi 85%”.  
 
Waziri Ummy hakusita kuwapongeza Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)  kwa kubuni mradi huo kwani utasaidia harakati za Serikali za kupunguza vifo vitokanavyo na  uzazi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuahidi kuwapa kipaumbele  kwenye huduma za mama na mtoto.
 
Kwa upande mwingine Waziri Ummy amewasisitiza watoa huduma za afya kote nchini kuzingatia taaluma, weledi , maadili na viapo vyao vya utumishi wa afya ili kuokoa maisha ya watu wanaofika kupata huduma kwenye vituo vyao.
 
Naye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lugano Kusiluka amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani  kwa kazi kubwa anayofanya katika kuimarisha huduma za afya ikiwemo huduma za mama na mtoto kwa kuwekezaji mkubwa wa miundombinu, vifaa tiba na ajira   katika  vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
 
Amesema UDOM wanao mpango mkakati wa miaka mitano kwa lengo la kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya ya jamii hivyo wanayo sababu ya kuonesha uwekezaji wa chuo kikuu hicho kinaleta tija kwa upande wa mradi huo lengo ni kuongeza  na kuboresha huduma jumuishi ya Kifua Kikuu (TB), UKIMWI na Malaria kabla na baada  ya kujifungua ili kumuheshimisha  mama.


 
Mradi jumuishi wa TB, UKIMWI na Malaria ni mradi wa miaka miwili  unafadhiliwa na Mfuko wa Global Fundi  na Liverpool School of Tropic of Medicine  kwa kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya  lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya ya mama kabla, wakati na baada ya kujifungua ili kusaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi .