Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

*INEC YAWATAKA WATENDAJI WA UBORESHAJI KUTUNZA VIFAA*


 

Na Mwandishi wetu, Kigoma
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetaka watendaji wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mkoani Kigoma kuhakikisha wanatunza vifaa vya uandikishaji ili vikaweze kutumika maeneo mengine nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegeke wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe 20 hadi 21 Juni,2024 Mkoani Kigoma.

“Kwa kusisitiza, ni muhimu kutekeleza majukumu yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini,” alisema Jaji Mwambegele.

Amesema kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivi kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili muhimu na amewataka kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili muweze kuyafanyia kazi wakati zoezi litakapokuwa limeanza.

Aidha, Jaji Mwambegele amesema matokeo bora ya zoezi hili yanategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi.

“Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa karibu na Tume wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo yeyote, msisite kuwasiliana na Tume,” alimema Jaji Mwambegele.

Mapema kabla ya kuanza mafunzo hayo, washiriki walikua kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Rose Kangwa.

Mafunzo hayo yanahusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration System - VRS) ili waweze kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura.

“Mafunzo haya, yanawajengea umahiri wa kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kisha nao watatoa mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,” alisema Jaji Mwambegele.

Aidha, Maafisa TEHAMA watapatiwa mafunzo maalum ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi (Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni.

Katika hatua nyingine, Jaji Mwambegele amewaambia watendaji hao kuwa  wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.

Jaji Mwambegele alitoa angalizo kwa mawakala hao kutoka vyama vya siasa kuwa  hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao vituoni.




Tume imetangaza uzinduzi wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura utafanyika tarehe 01 Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo Mgeni rasmi anataraji kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na kauli mbiu ya uboreshaji ni  “Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura Ni Msingi Wa Uchaguzi Bora”

MBUNGE NOLLO AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MIRADI MINGI YA MAENDELEO JIMBO LA BAHI

 
Na. Kadala Komba Bahi

 

Haya yamebainishwa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo wa Bahi Kenneth Nollo katika mkutano wa hadhara aliyofanya Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary Senyemule akisikiliza kero za wananchi  kata ya Bahi mtaa wa chuma ulete.
 
 "Mhe. Nollo alisema nampongeza rais Samia Hassan kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo Bahi, Tuna kila sababu ya kumshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kwajili ya miradi ya maendeleo kwa wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi"

Mhe. Nollo amesema  kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa katika wilaya ya Bahi ambapo miradi mingi na mikubwa ya maendeleo imeonekana ikiwemo miundo mbinu ya Barabara,  shule, Afya, Elimu hizi  zote ni juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia.


Mheshimiwa Mbunge wa jimbo wa Bahi Kenneth Nollo






Mkuu wa Mkoa Dodoma Rosemary Senyemule akisikiliza kero za wananchi  kata ya Bahi mtaa wa chuma ulete.
 

Mkuu wa wilaya ya Bahi Gift Msuya

Y
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Stewart Masima na mkuu wa wilaya ya Bahi Gift Msuya





Sosthenes Cosmas Mpandu Diwani Mpamantwa

Baadhi ya wananchi wakielezea kero zinazowakumba kwenye maeneo wanayoishi....


*TOFAUTI ZA DINI, SIASA ZISIWAGAWE WATANZANIA - DKT. BITEKO*


📌 Awataka waumini kushirikiana na Askofu Pangani

📌Serikali kuendelea kushirikiana na taasisi za dini nchini

📌 Rais Samia apewa tuzo kwa uongozi uliotukuka na kulinda amani

*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kudumisha amani, mshikamano na  upendo na kamwe wasigawanywe kwa sababu yoyote.

Amesema hayo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Robert Yondam Pangani wa Kanisa la Moravian Tanzania, Jimbo la Kusini Magharibi iliyofanyika leo Juni 2, 2024 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji mkoani Mbeya.

“Nimefurahi kusikia wewe ni mtu mtulivu na myenyenyekevu sana upokee jambo hili kwa amani, nina imani eneo lako la mahubiri litakuwa kubwa zaidi na sisi tutaendelea kukuombea kwa Mungu ili lile aliloweka ndani yako liweze kujitokeza”, amesema Dkt. Biteko.

Ametoa wito “Waumini wenzangu huyu si malaika ni binadamu itafika wakati atachoka naomba mumtie moyo, na msiache kumuombea na kumtii inawezekana kuna anayejua kuliko yeye lakini yeye amepewa fursa ya kuwaongoza nyinyi hivyo mumtii. Pia tusibaguane kwa dini zetu au vyama vyetu vya siasa, sisi tuliokaa hapa hatujatambuana kwa makabila yetu tunatambuana kwa utanzania wetu, wakati wote muhubiri amani na mtu yeyote mwenye shida aone Tanzania ni mahali salama” .

Pia, amemsii Askofu Pangani  kuwasikiliza watangulizi wake pamoja na Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania kwa kuwa wana heshima na hekima.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera amesema kuwa Mhe.Rais  Samia ameunganisha taasisi za dini na alichangia milioni 50 katika Kanisa la Moravian kwa ajili ya ujenzi wa ofisi mkoani Dodoma.

“ Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati naomba utusaidie katika  mgogoro wa kiwanja mkoani Dodoma ili waweze kujenga ofisi zao, Rais Samia yuko pamoja nao na ameunganisha taasisi za dini na ukiona taasisi hizi ziko pamoja ni jitihada zake hasa hapa Mbeya”, amesema Mhe. Homera.

Naye, Askofu Robert Yondam Pangani amesema kuwa amepokea kwa heshima na  kwa unyenyekevu mkubwa nafasi aliyopewa na anaahidi kuungana na viongozi wa dini kuhakikisha amani inadumu pamoja na kuimarisha ushirikiano na Serikali.

Askofu Pangani ametaja shughuli mbalinbali zinazofanywa na Kanisa hilo la  Moravian Jimbo la Kusini Magharibi ikiwemo kuwa na miradi inayotoa ajira kwa vijana na kutunza watoto yatima sambamba na kuwasomesha katika ngazi mbalimbali za elimu kuanzia awali, shule za msingi hadi vyuo vikuu.

“Watu 1,203 wenye mahitaji maalum wameendelea kupatiwa mahitaji mbalimbali na Kanisa ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa wajasiriamali, Kanisa pia linaungana   Serikali katika utunzaji wa mazingira ili kutunza vyanzo vyetu vya maji na kutatua changamoto ya maji kama ambavyo Rais wetu amedhamiria kumtua mama ndoo kichwani”, amesema Askofu Pangani.

Amesisitiza “Nampongeza Mhe. Rais Samia kwa mambo muhimu anayoendelea kufanya katika Taifa hili la kulinda amani pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali ya maji, barabara na umeme ambao uko nchi nzima mijini na vijini, na mimi naahidi kuwa Kanisa litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na tutaendelea kuwaombea viongozi wetu”.

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Kanisa la Moravian Duniani, Mchungaji  Erord Rupia  Simae wakati akisoma barua ya salamu kutoka kwa Rais wa Moravian Duniani, amesema kuwa wanampongeza Askofu Robert Yondam Pangani kwa kupata fursa ya kuongeza Kanisa hilo katika Jimbo la Kusini Magharibi na kuwa yeye ni mchungaji aliyepewa namba 380 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo duniani mwaka 1457 na pia amepewa namba 318 tangu Kanisa hilo kufanywa upya mwaka 1727.

Awali, Askofu Ezekiel Yona akimzungumzia
Askofu  Robert Yondam Pangani amesema kuwa amepewa nafasi na heshima hiyo  na Mungu hivyo akatende haki katika kutekeleza majukumu yake kwa kuwa watu wanataka kuona Askofu anayewarudisha watu kwa bwana na kuponya mioyo yao.

“Lazima tumtangulize Mungu ndani ya Ofisi ya Baba Askofu na kwa kuwa wewe umepitia ngazi nyingi katika kanisa hivyo kwa sasa unalijua kanisa vizuri zaidi ndani na nje. Ofisi yako ndio ya kujenga kanisa la kuabudu ndio na kweli”, amesisitiza Askofu Yona

Ameongeza kuwa Jimbo la Kusini Magharibi ni jimbo kubwa katika majimbo ya Kanisa la Moravian duniani na hivyo ashughulike nalo huku akiwaomba waamini wa kanisa hilo kutoa ushirikiano kwa Askofu huyo.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amepanda mti katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji kilichopo Mbeya ikiwa ni kumbukumbu ya ushiriki wake katika ibada hiyo.

Pia katika ibada hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepewa tuzo maalum ya utumishi uliotukuka, viongozi wengine waliopewa tuzo za utumishi uliotukuka pamoja na Naibu Waziri  Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, Spika wa Bunge na Rais wa Mabunge Duniani, Mhe. Tulia Ackson na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera.

Aidha, tendo la kumweka wakfu Askofu Robert Yondam Pangani limeongozwa na Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania, Conrad Nguvumali Sikombe pamoja na maaskofu wengine wa Kanisa hilo. Ibada hiyo pia imehudhuriwa na maaskofu kutoka nchi za Uingereza na Zambia.

Mwisho.