Na. Kadala Komba Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biblia cha Tanzania Askofu Mkuu Mark Walwa Malekana Amesema tunaamini taifa la leo na kanisa la leo limejengwa juu ya Watoto tusipofanya bidii kuwatahadharisha Watoto wa leo hakuna fyucha ya taifa wala fyucha ya watoto hivyo watoto wapatiwe umuhimu katika kupewa maandiko matakatifu katika kutekeleza hili tunawashukuru wadau mbalimbali ambao wamejitokeza kuchangia kuhusiana na Programu hii ya kupeleka Biblia nyingi magerezani pamoja na kwa watoto katika shule na vyuo vikuu pamoja na watoto walio uraiani kazi hii imefanikiwa sana Tunamshukuru Mungu Alisema .
hayo yamejiri wakati wa mkutano mkuu wa Chama cha Biblia Tanzania wa mwaka 2023 Mei 17/5/2024. katika Ukumbi wa Kanisa la KKKT Dodoma Mjini.
"Askofu Malekana Amesema Chama cha Biblia kimejipanga kuhakikisha kwamba Neno la Mungu ambalo ni Biblia linatawanywa kwa wingi nchini Tanzania kwa sasa tunakabiliwa na jambo ambalo ni mmomonyoko wa maadili watu wanapoteza yale maadili mazuri katika jamii tunalia na vijana sio kwa vijana tu hata watu wazima vitendo vya ulawiti katika jamii mambo mabaya kabisa utashangaa mtu mzima amelawiti mtoto wa miaka 2 mwaka 1 mambo ya ushoga ndoa za jinsia moja mambo haya yanaonyesha kwa kiwango kikubwa jinsi ambavyo maadili yanaporomoka ulimwenguni sisi tunaamini ya kwamba Dawa ya kuiponya jamii ni Neno la Mungu, hivyo chama cha Biblia kinajukumu kubwa la kuhakikisha kwamba wanachapisha Biblia kwa Lugha mbalimbali kiswahili na lugha mbalimbali za hapa Tanzania hili kuhakikisha kwamba Neno la Mungu likiwafikia watu maadili yatarudishwa mahali pake tutakuwa na taifa la Maana tutakuwa na Taifa la maana tutakuwa na Kanisa la maana na jamii ya maana. kwa sababu tunaamini kama kila Familia italiweka Neno la Mungu kipaumbele kwa sababu watoto na vijana na jamii inavyozaliwa na kukuzwa katika familia tunaamini ya kwamba kusaidia jamii ni mahali ambapo tunasaidia familia ni mkakati wetu kila familia ipate Neno la Mungu na inapopata Neno la Mungu italifundisha Neno la Mungu kwa watoto wanaozaliwa katika familia hiyo, na wao tumewatengenezea Biblia kwa namna yao,na watu wasio na uwezo wa kuona tumechapisha Biblia kwa uwezo wao moja na watu wenye matatizo ya viungo tumezingatia Alisema ".
Askofu Malekana Amesema kitabu kitakatifu Biblia ni Mwongozo kutoka kwa Mungu kwa kuwaongoza wanadamu wote hili wawe na maadili yanayostahili katika kuishi kwao hapa Duniani, hivyo kama cha cha Biblia kazi yake kubwa ni kutunza maandiko matakatifu katika usafi wake pamoja na kutafsiri Biblia kwa lugha mbalimbali ikiwemo lugha mama ya kiswahili na lugha za makabila mbalimbali pamoja na kutawanya Biblia kila mahali haswa magerezani pamoja na Watoto.
Kwaupande wake Mdhamini wa Chama cha Biblia Mhe.Jaji Joseph Sinde Walioba amesema tumekuwa tukijitahidi kwa uwezo wetu kutoa michango yetu kwa lengo la kupata Biblia za kutosha na katika hili tumepiga hatua na hizi Biblia zipo kwenye lugha mbalimbali hivyo inasaidia kuuneza Neno la Mungu katika hili niwahakikishie chama cha Biblia sisi ni kama watumishi wenu tutajitahidi kufanya kazi yenu iwe rahisi Alisema.
Naye Askofu Dr Stanley Hotay wa kanisa la Anglikan Arusha Amesema Chama cha Biblia kinawezeswa na makanisa makanisa yote ni wanachama cha Biblia na chama hichi japo ni mtoto wa kanisa hapa tunakubaliana tunaweza kukataana kwa siku za Ibada tunaweza kukataana kwa siku za ibada hata kwa vitu tunavyo viamini lakini kwenye Neno Biblia tunaunganishwa hivyo inatupasa chama hiki tukitie nguvu kwa pamoja.
" Askofu Hotay alisema wakati huu ni wakati mgumu ambao chama cha Biblia kinapitia kuliko wakati wowote wakati huu zipo Biblia Nyingi na chochote kinachozidi thamani inapungua ni lugha yakibiashara sasa tuna Biblia nyingi zipo kwenye Simu ambazohatujui nani amezitafsili kila mtu anaeweza kusoma hili ni janga kwa sisi ambao sio wasomaji wazuri wa biblia sisi ni wasikilizaji tu hivyo njia yoyote itanipeleka tu na waelekezaji wa Biblia wapo wengi hivyo nakisii sana chama cha Biblia kipite maeneno mbalimbali kueleza Biblia kamili ni hipi Alisema.
Anaye fuatia ni Askofu Amos Muhagachi Makamu mwenyekiti wa chama
Mwisho ni Dkt Alfred Kimonge Katibu Mkuu wa chama
Katibu Mkuu Dkt Alfred Kimonge akizungumza mipango mikakati ya chama cha Biblia Tanzania |
|