Na. Kadala Kuomba Dodoma
Hayo yamejiri jijini Dodoma katika shughuli ya upandaji miti shule ya msingi uhuru
Dkt. Benson Ndiege Mrajis wa Vyama vya Ushirika amesema tunapozungumzia mazingira ni swala la kidunia ni swala la kiulimwengu kwamaba mataifa yote ikiwemo Tanzania tunashiriki kuhakikisha kwamba tunaboresha mazingira kwa masilahi ya mwanadamu ambao wanaishi kwenye Dunia hii.
"Kwa nchi yetu ya Tanzania Agenda ya mazingira ni Agenda kubwa na imepewa nafasi kubwa tumeona viongozi wetu wa kitaifa akiwemo Mh.Rais waziri Mkuu na Makamu wa Rais wakishiriki na kutuhamasisha kwenye maeneo mbalimbali kulinda mazingira hasa kwenye matukio kama haya ya upandaji miti hasa kwenye misimu ya mvua kama sasa hivi"
Aidha Dkt. Benson Ndiege Amesema tunaunga mkono jitihada za serikali katika kurinda mazingira na kuboresha mazingira ndio maana leo tumekusanyika hapa kwa lengo moja tu la kupanda miti, sisi kama Tume ya ushirika tunasimamia vyama vya ushirika nchini takribani elfu 7 mia nne na zoezi hili ni uzinduzi wa upandaji wa miti nchi nzima kwenye vyama vya ushirika ni zoezi endelevu Alisema.
Kwa upande wake Leonard Bilomo Afisa misitu Daraja la pili amesema tukio la leo la upandaji miti kwenye shule hii ni kupendezesha na kutengeneza mazingira ya eneo hili pia wanafunzi waweze kufaidika na matunda ya miti hii.
Kwa niaba ya Wanafunzi wa shule hiyo Abdul Ramadhani Ameishukuru Tume ya Ushirika kwa Elimu namna Bora ya kupanda miti na kuitunza tunayo furaha kwa kuletewa miti kwenye shule yetu, sisi kama wanafunzi tutaitunza hii miti kwa sababu miti inafanya shule iwe na mwonekano mzuri na vivuli vya kupumnzikia.